Friday, June 24, 2011

DARAJA LA MUNGU RUNGWE

Wilaya Rungwe inavivutio vingi vya utalii, moja ya kivuti ambacho ni maajabu makubwa kwa dunia nzima ni Daraja la Mungu ambambalo unalitazama kwenye picha hiyo kama Umoja wa watangazaji mkoa wa Mbeya tunawakaribisha wadau mbalimbali kuja mkoa wa Mbeya na kutembelea vivutio hivyo muhimu na vyenye historia za ajabu hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Thursday, June 23, 2011

AKAMATWA NA KIGANJA CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI WAKE


JEMSI MAMBICHI mkazi wa kijiji cha Asamba wilayani Mbozi amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya akiwa na kiganja cha mtoto mchanga.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa nyumbani kwake ambapo kiungo hicho kilikuwa kimechimbiwa chini pembezoni mwa mlago wa chumbani kwake.

Kiungo hicho kimehifadhiwa hospitali ya Vwawa Mbozi kwaajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

Aidha kamanda NYOMBI amesema ELISHA AHONGA mwanafunzi wa shule ya msingi Sumbalwela amefariki dunia baada ya kupigwa na jiwe kichwani na NESTO MKONDYA mwanafunzi mwenzake wakati wakicheza mpira wa miguu shuleni hapo, mtoto huyo amekamatwa kwaajili ya uchunguzi zaidi.

WAFANYABIASHARA WASAMAKI MBEYA WATUMIA DAWA AINA YA ACCARICIDES KUHIFADHIA SAMAKI

Afisa afya mkoa wa Mbeya PETER MEREKI amesema kuwa wafanyabiashara wa samaki wa bichi watakaye bainika wanatumia dawa aina ya Accaricides ambayo inatumika kwa kilimo kuhifadhia samaki hao atachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuondoa hatari ya kiafya inayoweza kuwapata watumiaji wa samaki hao.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano na bomba fm na kusema kuwa mikoa ambayo inaongoza kwa wafanyabiashara kutumia dawa hiyo ni  Rukwa, Katavi na Mbeya


Wakati huohuo amewataka wananchi kutoa taarifa za haraka kwa vyombo vya sheria endapo watabaini kuwepo kwa wafanyabiashara wanaotumia dawa aina ya ACCARICIDES kwenye maeneo yao ili kuweza kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitumia dawa hizo kwa madai kuwa inasaidia kuwakinga samaki wabichi wasiharibike mapema hata hivyo dawa hiyo ni sumu kwa afya ya binadamu.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HII LEO.

Leo ni siku ya wajane na Wagane Duniani ambapo wajane hupata fulsa  ya kutafakari majukumu muhimu walio achiwa na waumezao.

Akiongelea maadhimisho hayo wakili kutoka kituo cha msaada wa sheria (NOLA) Bwana SIMON NG’WIGULI amesema kisheria Mjane ni mrithi na mmiliki wa kwanza wa mali za Marehemu

Ameongeza kuwa mkoa wa Mbeya ni mmoja kati ya mikoa ambayo wajane wameathirika sana

Wakati huohuo ameimba serikali kuiadhimisha siku ya wajane kama inavyofanya kwenye maadhimisho mengine ili kutoa fulsa kwa wajane kujua haki zao za msingi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HII LEO.

Saturday, June 18, 2011

Jaji Mkuu Othman Chande (kushoto) akionesha vitabu vya haki na utii bila shuruti baada ya kuzindua kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu utii wa sheria bila shuruti katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi , Said Mwema.

HABARI ZAIDI

VIONGOZI wa siasa nchini wametakiwa kupanda mbegu za maadili mema kwa wafuasi wao, huku wao wenyewe wakionesha mfano wa kuwa mstari wa mbele kutii sheria za nchi.

Aidha, wametakiwa kuelewa, kwamba tafsiri ya kupenda nchi si kufanya harakati za kuchochea ukiukwaji wa sheria.

Hayo yalisemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu utii wa sheria bila shuruti uliofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

Alisema uzinduzi wa kampeni hizo umekuja kwa wakati mwafaka, hasa katika kipindi ambacho nchi imekumbwa na matukio ya wananchi kujifanya wanadai haki, lakini bila kuzingatia wajibu walionao kisheria.

Katika hotuba yake, aliyoitoa mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwamo makamanda wa Polisi wa mikoa yote nchini, wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wa asasi za kiraia, alisisitiza juu ya utekelezaji wa kampeni hiyo kwa vitendo, kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Jaji Mkuu pia aliwataka viongozi wa dini kuelewa kwamba wana wajibu mkubwa wa kuongoza dhamira za wafuasi wao kutenda mema, kuhimiza na kulinda maadili ya jamii kwa ajili ya kujenga amani na umoja wa kitaifa.

Kwa upande wa asasi za kiraia, alisema nazo zina jukumu kubwa kwa umma wa Watanzania wanaopaswa kupewa elimu chanya ya uraia na uzalendo, huku wakitimiza maadili mema ya kitanzania.

Akimkaribisha Jaji Mkuu kuzindua kampeni hiyo, IGP Mwema alisema kampeni hiyo itakayosambaa hadi ngazi za mashina, inalenga kuwaamsha na kuwapa hamasa Watanzania kuirejea misingi ya uwajibikaji katika harakati za kudumisha amani, usalama na utulivu, kama mtaji wa kujiletea maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.

RAIS MSTAAFU WA ZAMBIA FREDERICK CHILUBA AMEFARIKI DUNIA

Rais mstaafu wa Zambia Frederick Chiluba(pichani) amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Moyo na Ini,

Msemaji wa aliyekuwa rais huyo bwana Emmanuel Mwamba alieleza.Rais huyo alifariki baada ya maumivu makali ya tumbo aliyokuwa akiyasikia.

Alifariki ndani ya dakika tano tu baada ya maumivu hayo usiku wa manane nyumbani kwake alipokuwa akiishi.

Habari zilizotangazwa na kituo cha television cha taifa nchini Zambia zinaeleza kuwa Rais Chiluba alikuwa ni mzima na afya siku ya jana lakini hali yake ilibadilika kuanzia saa sita na nusu za usiku na arifariki dunia muda mchache tangu alipokuwa akilalamikia kusumbuliwa na tumbo. 

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKEMEA UFUGAJI HOLELA WA MIFUGO MBARALI


ZAIDI ya Shilingi 73,000,000 zimekusanywa na mamlaka ya hifadhi ya taifa TANAPA katika kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi Mei mwaka huu  kufuatia malipo ya adhabu ya wafugaji kuingiza mifugo katika hifadhi ya Ruaha upande wa eneo la Ihefu wilayani Mbarali.
  
Kwa mujibu wa kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ruaha Dodwell Ole Meing’ataki baadhi ya wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo hususani ng;ombe katika maeneo ya hifadhi jambo ambalo ni kinyume na sheria hivyo TANAPA kulazimika kuwawajibisha wanapowakamata.
  
Meing’ataki alisema mwezi oktoba mwaka jana mamlaka ilikusanya kiasi cha shilingi milioni moja na mwezi disemba milioni 19, lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda mifugo zaidi ikaendelea kuingizwa ndani ya hifadhi.
  
Alisema mnamo Januari mwaka huu Tanapa ilikamataa mifugo 500 na kutoza faini ya jumla ya shilingi milioni 12,April wakakamataa mifugo 1600 na kutoza zaidi ya shilingi milioni 30 na mei ikakamatwa mifugo 700 ambapo zilipatikana milioni 11.
  
Kaimu mhifadhi mkuu huyo alisema makundi ya mifugo yamekuwa yakiingizwa hifadhini nyakati za usiku ambapo ni vigumu kufanya doria kwa kutumia helkopta na inapofika asubuhi mifugo hiyo hurejeshwa katika maboma ya wafugaji.
  
Hata hivyo alifafanua kuwa tatizo la wafugaji kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi linaonekana kusababishwa na makundi makubwa ya mifugo inayoonezeka katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ambapo inasadikiwa wafugaji waliohamishwa kupisha hifadhi wanarejea katika vijiji hivyo.
  
Kwa upande wake mkuu wa mkoa John Mwakipesile aliipongeza TANAPA kwa kutoza faini kwa wafugaji wakaorofi akisema kazi hiyo ni kubwa na pasipo kufanya hivyo wafugaji wangesababisha kupotea kabisa kwa eneo oevu la Ihefu lililo chanzo kikubwa cha maji yam to Ruaha yaliyotegemeo katika bwawa la kuzalisha nishati ya umeme la Mtera.

Mwakipesile alisisitiza mamlaka nyingine zilizo karibu na hifadhi hiyo kuona haja ya kusaidia mikakati ya TANAPA katika kulinda hifadhi hiyo huku akiutaka uongozi wa serikali ya wilaya ya Mbarali kuwachukulia hatua viongozi wa vijiji wanaopokea wafugaji waliohamishwa kutokana na kuwa na makundi makubwa ya mifugo.


Monday, June 13, 2011

WAZEE WA MSIMBAZI KATIKA PICHA YA PAMOJA



BAO pekee lililofungwa dakika ya saba na mshambuliaji Mussa Hassan 'Mgosi', liliifanya timu ya Simba kuanza vizuri kampeni yake ya kutinga hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho (CAF) kwa kuifunga DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) bao 1-0.

Mchezo huo uliopigwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuhuriwa na mashabiki wachache, ulikuwa na burudani ya aina yake kwa kila timu kucheza vizuri lakini kivutio pekee kilikuwa kwa beki wa Motema Pembe, Feugang Takudjo ambaye alikuwa akirusha mipira kwa staili ya aina yake.

Katika mchezo huo, timu zote zilianza kwa kasi kwa kushambuliana kwa zamu na Motema Pembe, walionekana kutakata zaidi kwa mtindo wao wa kupiga pasi nyingi na kushambulia kwa kushtukiza.

Pamoja na hali hiyo, Simba ilipata faulo dakika ya saba baada ya Emmanuel Okwi, kufanyiwa madhambi ambapo Mgosi alikwamisha mpira wavuni kutokana na mpira uliopigwa na Mohamed Banka, aliyeunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Okwi.

Baada ya kufungwa bao hilo, Motema Pembe iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 17, Ilongo Ngasanya alishindwa kukwamisha mpira wavuni kutokana na mpira uliorushwa na Takudjo, kuwachanganya mabeki wa Simba.

Beki Takudjo alikuwa kivutio kwa kuwa kabla ya kurusha mpira alilazima kubinuka sakarasi, kitendo kilichowachanganya waamuzi na kufikia wakati kujadiliana juu ya mtindo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikionekana kutafuta bao, lakini dakika ya 63, Bokota Labama wa Motema nusura aisawazishie timu yake bao lakini alishindwa kuunganisha krosi iliyopigwa na Salakiaku Matonda.

Motema ilizidisha presha kwa Simba na dakika mbili baada ya tukio hilo, beki Haruna Shamte wa Simba alioneshwa kadi ya pili ya njano na baadaye nyekundu na mwamuzi Solomon Wakoma, kutoka Nigeria na kutoka nje kwa kumchezea vibaya Matonda.

Wakati mchezo ukiendelea, dakika ya 68 mwamuzi Wakoma alijichanganya baada ya kupuliza filimbi ya kuotea kwa wachezaji wa Motema.

Simba ilijaribu kutuliza mashambulizi ya wapinzani wao kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kutumia mipira mirefu, lakini haikuzaa matunda kwani mabeki wa Motema walikuwa makini kuondosha hatari hizo.

Zikiwa zimebaki dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho kupulizwa, Diavita Dama aliyeingia badala ya Landu Makela alikosa bao la wazi kwa kushindwa kuunganisha krosi ya Ilongo.

Simba: Juma Kaseja, Shamte, Amir Maftah, Juma Nyosso, Yondani, Amri Kiemba, Nicco Nyagawa, Juma Jabu, Okwi, Mgosi/Salum Kanoni na Banka.

WATANGAZAJI KUTOKA REDIO ZA Bomba Fm-Mbeya, Tbc Fm-Ruvuma, Kitulo Fm, Up landas Fm, Nuru Fm na Ebony Fm

Unywaji wa pombe si mbaya kibaya ni unywaji wa pombe kupita uwezo wako kwani humfanya mtu kukosa ustaharabu na muda mwingineHudhoofisha mwili, husababisha tatizo la Fifo, Matatizo ya Figo na kuleta utegemezi katika maisha.Jamani tutambue kuwa unywanji wa pombe kupita kiasi ama utumiaji wa dawa za kulevya ni hatari kwa afya yao.
Watangazaji hawa wanasema kuwa jamanii CHONDE CHONDE ULEVI NOMAAAAAA!!!!

Rais Dk.JAKAYA KIKWETE akiteta jambo na mfalme Muswati wa 3

Rais Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Mfalme Mswati III wakati wa ufunguzi wa mkutano wa SADC unaofanyika Santon, Johannesburg, Afrika Kusini. Katikati aliyesimama ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Anthony Itatiro.

SPIKA WA BUNGE ANNA MAKINDA

Spika wa kwanza wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwanamke ANA MAKINDA Akiingia Bungeni kwaajili ya kufungua bunge la 10 kikao cha 4, Kikakao ambacho kimetoa sura halisi ya Mtanzania katika Kipindi cha mwaka wa Fedha 2011/2012.Huku bajeti iliyosomwa na waziri wa Fedha na Uchumi June 8 mwaka huu bajeti ambayo imetoa vipaumbele vya Serikali kwa mwaka huu kuwa ni 1.Umeme 2.Maji 3.Miundombinu ya usafiri na usafirishaji-Reli, Barabara,Bandari,Viwanja vya ndege na mkongo wa Taifa 4.Kilimo na Umwagiliaji 5.Kupanua ajira kwa sekta binafsi na Umma