Friday, July 22, 2011

UKWELI WAPATIKANA KWA DIWANI WA CHADEMA KUHAMIA CCM - NZOVWE MBEYA

Zikiwa zimepita siku 3 tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedanganya Umma katika mkutano wake kwa kusema Diwani wa kata ya Nzovwe EZIRONI MWAKALOBO kupitia Chadema amejihuzulu na kuhamia CCM hatimae viongozi hao wamebadilisha usemi kwa kukubali kuwa kilichoongelewa ni kweli.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya mjini JOHN MWAMBIGIJA amesema pamoja na jitihada za uongozi wa chama chake kushinikiza kukanusha barua ya kujihuzulu wadhifa wake bado EZIRONI MWAKALOBO ameendelea na msimamo wake wa kung’atuka madarakani.

Aidha MWAMBIGIJA amesema mpango wa CHADEMA hivi sasa ni kujipanga katika kuhakikisha wanachukua tena kiti cha Udiwani kata hiyo mara baada ya kutangazwa kwa uchaguzi mdogo.

Hata hivyo siku ya kukanushwa kwa kauli za Chama Cha Mapinduzi Diwani EZIRONI MWAKALOBO alisema kuwa uamuzi wa kujizulu umetokana na mvutano uliopo ndani ya Chama Chake.


WANAFUNZI WASHINDWA KUENDELEA NA MASOMO WILAYANI CHUNYA
Wanafunzi 400 waliotarajiwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari wilaya ya Chunya mkoani Mbeya mwaka huu wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu zisizojulikana.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo MAURCE SAPANJO amesema wanafunzi hao licha ya kufaulu kwa viwango vizuri hawakuweza kuendelea na masomo na kwamba wazazi wa watoto wameshindwa kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kufanikisha kuwarejesha wanafunzi hao masomoni.

Amesema uchunguzi uliofanywa na halmashauri hiyo umebaini kuwa watoto wengi wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kukimbilia kwenye shughuli za madini.

Katika taarifa ya mkoa wa Mbeya iliyosomwa kwa Waziri mkuu MIZENGO PINDWA mwaka 2008 alipofanya ziara mkoani hapa ilidai kuwa wanafunzi 703 walikatiza masomo kwa sababu ya utoro na mimba.


TCRA YATOA MISAADA YENYE THAMANI YA MIL 2.5 WILAYANI CHUNYA.
Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Imetoa msaada wenye thamani ya Shilingi milioni kumi na mbili na nusu kwa ajili ya kununua computer, printer na photocopy katika shule za msingi na sekondari wilayani chunya.

Naibu mkurugenzi wa TCRA bwana VICTOR NKYA amesema misaada hiyo imetolewa ili iwawezesha wanafunzi na waalimu wa shule hizo kuendana na sayansi na teknolojia.

Wakati huohuo ameitaka Serikali kuongeza nguvu katika usambazaji wa vifaa vya teknolojia mshuleni ili kuwawezesha waalimu kuendana TEHAMA.

Shule zilizopata misaada hiyo ni Chunya kati, Chokaa, Mapogoro na Makongorosi ambapo kila shule imepata Computer moja na Printer moja.


MAUAJI YA KIMYA MKOANI MBEYA NI KAMA WIMBO WA TAIFA.
MBAGALE NDUNGA mwenye umri wa miaka 73 mkazi wa Chemchem Uyole ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiofahamika kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mchawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema marehemu alikuwa akituhumiwa kuhusika na matukio ya Uchawi ukiwemo wizi wa mazao shambani kwa njia za kishirikina.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na upelelezi wa kuwabaini wahusika wa mauaji hayo unaendelea.

Zimewekwa na UKURASA MPYA HUU http://ukurasampyahuu.blogspot.com/ 

No comments:

Post a Comment