Friday, July 22, 2011

JAIRO APEWA LIKIZO YA MALIPO KUPISHA UCHUNGUZI WA RUSHWA DHIDI YAKE

 Katibu Mkuu, Phillemon Luhanjo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo alitangaza rasmi kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kufuatia kashfa zinazomuandama hivi sasa.
Picha ya Kukopi katika moja ya gazeti, Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, amesimamishwa kazi rsmi kufuatia kutangazwa rasmi habari hizo na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemo Luhanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma Julai 21 mchana.

MAGARI MAWILI YATEKETEA KWA MOTO MARA BAADA YA KUGONA USO KWA USO

 HIVI NDIVYO GARI LA HOOD LINAVYOONEKANA BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO
HAPA NI GARI LA HOOD NA GARI LA MIZIGO LIKIWAKA MOTO MARA BAADA YA KUGONGANA KATIKA ENEO LA MIKUMI MKOANI MOROGORO

BASI LA HOOD LATEKETEA KWA MOTO LAUA 5 NA KUJERUHI 41

hivi ndivyo hali ilivyotokea baada ya basi la Hood lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Arusha,lilipogongana uso kwa uso na lori la mizigo lilolokuwa na mafuta ya kula tani 24 kutoka Morogoro kwenda Songea kwenye barabara iliyopo ndani ya hifandi ya Taifa ya Mikuki,mkoani Morogoro.watu watano walifariki na 41 kujeruhiwa.

UKWELI WAPATIKANA KWA DIWANI WA CHADEMA KUHAMIA CCM - NZOVWE MBEYA

Zikiwa zimepita siku 3 tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimedanganya Umma katika mkutano wake kwa kusema Diwani wa kata ya Nzovwe EZIRONI MWAKALOBO kupitia Chadema amejihuzulu na kuhamia CCM hatimae viongozi hao wamebadilisha usemi kwa kukubali kuwa kilichoongelewa ni kweli.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya mjini JOHN MWAMBIGIJA amesema pamoja na jitihada za uongozi wa chama chake kushinikiza kukanusha barua ya kujihuzulu wadhifa wake bado EZIRONI MWAKALOBO ameendelea na msimamo wake wa kung’atuka madarakani.

Aidha MWAMBIGIJA amesema mpango wa CHADEMA hivi sasa ni kujipanga katika kuhakikisha wanachukua tena kiti cha Udiwani kata hiyo mara baada ya kutangazwa kwa uchaguzi mdogo.

Hata hivyo siku ya kukanushwa kwa kauli za Chama Cha Mapinduzi Diwani EZIRONI MWAKALOBO alisema kuwa uamuzi wa kujizulu umetokana na mvutano uliopo ndani ya Chama Chake.


WANAFUNZI WASHINDWA KUENDELEA NA MASOMO WILAYANI CHUNYA
Wanafunzi 400 waliotarajiwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari wilaya ya Chunya mkoani Mbeya mwaka huu wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu zisizojulikana.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo MAURCE SAPANJO amesema wanafunzi hao licha ya kufaulu kwa viwango vizuri hawakuweza kuendelea na masomo na kwamba wazazi wa watoto wameshindwa kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kufanikisha kuwarejesha wanafunzi hao masomoni.

Amesema uchunguzi uliofanywa na halmashauri hiyo umebaini kuwa watoto wengi wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kukimbilia kwenye shughuli za madini.

Katika taarifa ya mkoa wa Mbeya iliyosomwa kwa Waziri mkuu MIZENGO PINDWA mwaka 2008 alipofanya ziara mkoani hapa ilidai kuwa wanafunzi 703 walikatiza masomo kwa sababu ya utoro na mimba.


TCRA YATOA MISAADA YENYE THAMANI YA MIL 2.5 WILAYANI CHUNYA.
Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) Imetoa msaada wenye thamani ya Shilingi milioni kumi na mbili na nusu kwa ajili ya kununua computer, printer na photocopy katika shule za msingi na sekondari wilayani chunya.

Naibu mkurugenzi wa TCRA bwana VICTOR NKYA amesema misaada hiyo imetolewa ili iwawezesha wanafunzi na waalimu wa shule hizo kuendana na sayansi na teknolojia.

Wakati huohuo ameitaka Serikali kuongeza nguvu katika usambazaji wa vifaa vya teknolojia mshuleni ili kuwawezesha waalimu kuendana TEHAMA.

Shule zilizopata misaada hiyo ni Chunya kati, Chokaa, Mapogoro na Makongorosi ambapo kila shule imepata Computer moja na Printer moja.


MAUAJI YA KIMYA MKOANI MBEYA NI KAMA WIMBO WA TAIFA.
MBAGALE NDUNGA mwenye umri wa miaka 73 mkazi wa Chemchem Uyole ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiofahamika kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mchawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema marehemu alikuwa akituhumiwa kuhusika na matukio ya Uchawi ukiwemo wizi wa mazao shambani kwa njia za kishirikina.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na upelelezi wa kuwabaini wahusika wa mauaji hayo unaendelea.

Zimewekwa na UKURASA MPYA HUU http://ukurasampyahuu.blogspot.com/ 

Thursday, July 21, 2011

VIONGOZI WA NCHI MBILI WAKISHUHUDIA MAWAZIRI WAO WAKIBADILISHANA MIKATABA

Mawaziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na Tanzania Bernard Membe na Bi. Maite Nkoana Mashabane wakibalishana mikataba ya kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano (Bi-National Commission) kati ya nchi hizo mbili muda mfupi baada ya kusaini katika ikulu ya Afrika ya Kusini jijini Pretoria jana huku marais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Jackob Zuma wakishuhudia.

RAIS KIKWETE ZIARANI AFRICA YA KUSINI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Ulinzi la Afrika ya Kusini wakati wa mwanzo wa Ziara yake Rasmi ya kitaifa nchini Afrika ya Kusini hivi karibuni.

NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA MATAIFA WAPINGA BARAZA KUU LA USALAMA

NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA MATAIFA WAPINGA BARAZA KUU LA USALAMA KUPEWA DHAMANA YA KURATIBU NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI (1)

New York
Wakati tishio la mabadiliko ya tabia nchi likiwa Dhahiri kwa hatima ya  mataifa mbalimbali  yakiwamo  yale ambayo ni visiwa. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepinga kwa mara nyingine, juhudi za  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa za  kushinikiza  kupewa dhamana ya  kuratibu  athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa  siku nzima ya jumanne, Baraza hilo ambalo liko chini ya Uraisi wa Ujerumani kwa mwezi huu wa Saba,   lilikuwa na mjadala wa wazi  kuhusu   Udumishaji wa amani na usalama wa kimataifa; madhara ya  mabadiliko ya tabia nchi.

Lengo la  majadiliano   hayo  pamoja na mambo mengine,yalikuwa ni kwa Baraza  hilo kushinikiza  liwe na  uwezo wa kuratibu na  kushughulikia uwezekano wa ukosefu wa amani na usalama utakaosababishwa na madhara ya  yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.

Karibu kila Balozi anayeiwakilisha nchi yake katika UM ,wakiwamo baadhi ambao nchi zao ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama maarufu kama P5, waliochangia   majadialiano hayo, walisema  ingawa  wana kubali  ukweli kwamba madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, yanatishia usalama na amani ya jumuia ya kimataifa, bado Baraza hilo haliwezi kuwa na  dhamana ya kulijadili , kulitolea maamuzi au maelekezo suala hilo.

Baadhi ya  hoja zilizotolewa na wazungumzaji hao ni kwamba,  ikiwa  Baraza Kuu la Usalama  litapewa dhamana hiyo.  Siyo tu  kwamba ,halina wataalam  katika eneo hilo, lakini litakuwa linaingilia majukumu, dhamana na wajibu wa vyombo  vingine vya UM  ambavyo hasa ndivyo vilivyokasimiwa  kulishughulikia  tatizo hilo. Na kusisitiza  kuwa viachwe vyombo hivyo vifanye kazi yake

Majadiliano hayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambaye pamoja na kuwasilisha taarifa yake  kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia alisema, athari za mabadiliko hayo zipo wazi kabisa na wala hazina mjadala.

Hata hivyo akasema,  yeye anadhani  kutokana na tishio la kiusalama,  na ustawi wa maendeleo  na uhai wa mataifa mbalimbali na watu wake. Baraza  Kuu la Usalama,  linapashwa pia kupewa dhamana ya  kuratibu  athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Akichangia majadiliano hayo, mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika UM, Balozi Ombeni Sefue, alisema , Serikali ya  Tanzania  inatambua kwamba kuna  kipengele  cha usalama katika mabadiliko ya tabia nchi,  kipengele ambacho  pia kiko   karibu katika kila  jambo   katika dunia hii.

  Hata hivyo hatujayaleta hayo mengine   kujadiliwa katika Baraza Kuu la Usalama la UM kama tunavyotaka kufanya kwa hili. Ujumbe wangu unaamini kwamba,  mabadiliko ya tabia nchi yanashughulikiwa kwa ukamilifu na vyombo vya msingi vya   UM. Vyombo ambayo  vimepewa dhamana  ya kushughulikia  suala la Maendeleo Endelevu ” akasema Balozi  Sefue.

Na kuongeza. “Mwaka 2007 tulikuwa na majadiliano kama haya, na  maoni ya wajumbe wengi waliochangia majadiliano yale yalikuwa,  Baraza  la Usalama lijiepushe kuingilia dhamana za taasisi nyingine za UM kama vile  Mfumo wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (UNFCCC ) na  Baraza la Uchumi na Mandeleo ya Jamii  ( ECOSOC).

Aidha Balozi Sefue amasema,  Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine inatambua ukubwa wa athari za mabadiliko ya tabia  nchi kwa   visiwa  vilivyoko katika  bahari ya Pasifiki.

Lakini akasema ,  tishio la kutoweka  kwa nchi hizo, tishio ambalo pia linaweza kuzalisha wakimbizi ,haliko kwa visiwa hivyo tu. Bali ni tishio hata kwa Tanzania n ambayo nayo ina visiwa   ambavyo  vimo hatarini  kutoweka.

Kwa hiyo akasema , ndiyo maana Tanzania imekuwa ikisisitiza na kusimamia kwamba  majadiliano kuhusu tatizo la mabadiliko ya tabia nchi na athari zake lijadiliwe zaidi katika ngazi ya  kimataifa kupitia  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  ili kupata  ufumbuzi wa kudumu.

Akasisitiza kuwa, kwa kutenga tatizo la mabadiliko ya tabia nchi na kuliingiza katika Baraza Kuu la Usalama, kunaweza kufifisha jitihada zote  ambazo zimekwisha kufanyika na hivyo kutokamilisha majadiliano  yanayo simamiwa na  UNFCCC.

Halikadhalika , mwakilishi huyo wa Tanzania  amerejea wito uliotolewa na wajumbe wengine wa kutaka nchi maskini kama Tanzania  na zile ambazo zimo katika hatari kubwa ya kutoweka, na  zile ambazo zimeonyesha nia thabiti ya  kudhibiti hewa ukaa na uhifadhi wa  mazingira kwa kupanda miti ya ziada. Zisaidiwe kwa hali na mali na mataifa  yaliyoendelea ambayo hasa ndiyo  chanzo kikubwa cha mabadiliko ya tabia nchi.