Thursday, July 21, 2011

KILIMO KWANZA KATIMA MSIMU WA NANENANE MKOANI MBEYA 2011

Imeelezwa kuwa huenda kuwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi katika viwanja vya maonesho ya kilimo nane nane mwaka huu likawa kubwa kuliko miaka iliyopita kutokana na mgao wa umeme unaendelea hivi sasa.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka jiji la Mbeya Injinia SIMIONI SHAURI wakati akijibu swali lililoulizwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya kuhusu suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi katika viwanja hivyo.

Awali katika swali lake la msingi mkuu wa mkoa wa Mbeya JOHN MWAKIPESILE alitaka kuelezwa namna ambavyo mamlaka ya maji safi imejipanga kutoa huduma ya maji safi katika kipindi chote cha maonesho.

Maonesho ya kilimo NANE NANE yanatarajia kufanyika kikanda mwaka huu mkoani Mbeya kuanza agosti mosi hadi nane mwaka huu katika viwanja vya JOHN MWAKANGALE vilivyo kata ya Isyesye jijini hapa yakiwa na kauli mbiu ya KILIMO KWANZA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA na TUNAZIDI KUSONGAMBELE.

MGOMO BARIDI WA VIONGOZI MJI MDOGO WA TUNDUMA WILAYANI MBOZI.
Imedaiwa kuwa mji wa Tunduma wilaya Mpya ya Momba huenda ikakabiliwa na vurugu baada ya baadhi ya viongozi wa madereva wa magari ya mizigo kukubali kwenye mkutano jana kuendelea na kazi ya usafirishaji.

Habari zilizotufikia kwenye chumba chetu cha habari zinadai kuwa wasiwasi wa vurugu hizo umeanza kuonekana baada ya madereva wa magari makubwa kulazimishwa kuondoa magari katika kituo kikuu cha maroli cha Sogea -Tunduma na kuendelea na safari.

habari zaidi zinadai kuwa Madereva hao wanataka mgomo kuendelea na hivyo kuanza kuwashambulia viongozi wao wakidai wamewasaliti baada ya kukubaliana na mkuu wa mkoa wa Mbeya kusitisha mgomo wao wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.

Mwenyekiti wa muda wa Madereva wa maroli yanayofanya safari zake nje ya nchi MOHAMED FIKIRI amesema msimamo wa chama chao ni kuendelea na mgomo nchi nzima.

FOREST JIJINI MBEYA. KAMATI YA NANE NANE
Hofu ya wamiliki wa vibanda vilivyopo pembezoni mwa uwanja wa nane nane Mbeya kuibiwa bidhaa zao imetajwa kuwa sababu ya wamiliki hao kushindwa kumalizia ujenzi wa vibanda vyao.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya EVANSI BALAMA katika kikao cha kamati ya maonesho ya kilimo NANE NANE kilichowakutanisha wakuu wa mikoa mine ya kanda ya nyanda za juu kusini ambayo ni IRINGA, RUKWA, RUVUMA na MBEYA.

Pamoja na maelezo ya wamiliki wa vibanda hivyo mkuu wa wilaya amewataka kukamilisha ujenzi wa vibanda vyao kabla ya Serikali kufuta umiliki kwao na kuwapatia wengine.

Naye meya wa jiji la Mbeya ATANASI KAPUNGA amesema kuwa halmashauri haitoweza kuvumilia kuona uchafu wa majengo pembezo mwa barabara hivyo italazimika kuvunja endapo havitaendelezwa.

Mkutano wa leo umelenga kutatua changamoto zilizopo ndani ya uwanja wa maonesho ya kilimo nane nane ili kuwayafanya kuwa bora zaidi.

 Imewekwa na http://ukurasampyahuu.blogspot.com/ UKURASA MPYA HUU  

Wednesday, July 20, 2011

MSIMU WA NANENANE MKOANI MBEYA 2011

VIWANJA VYA MWAKANGALE – NANENANE – UYOLE

Wakulima 50 kutoka halmashauri za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki katikakuonesha shughuli za kilimo katika meonesho ya wakulima NANENANE ambayo yanatarajia kuanza agasti mosi mwaka huu kwenye uwanja wa JOHN MWAKANGALE.

Meneja wa uwanja wa maonesho hayo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana KASILATI MWAKIBETE amesema kuwa halmashauri zote zimethibitisha ushiriki wao na kwamba hatua inayoendelea hadi sasa ni ya kushindanisha wakulima katika shughuli za kilimo.

Kauli mbinu ya maonesho ya kilimo nanenane mwaka huu KILIMO KWANZA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBELA.
CHUNYA MKOANI MBEYA.

Wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilayani Chunya Mkoani Mbeya wako hatarini kupoteza maisha kutokana na wazazi kuwapeleka watoto wenye ujauzito kwa waganga wa jadi ili kutoa mamba zao.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari kwa msaada wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umebaini kuwa vitendo hatari vimekuwa vikifanywa  kwa siri kubwa kati ya wazazi NA WAGANGA HAO WA JADI.

Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali teule ya Mwambani, wilayani hapo, Dakta BENANGODI KUSENGE amethibitisha kufanyika kwa vitendo hivyo ambapo tangu Mwaka jadi hadi mwaka huu wasichana watano wakiwemo wanafunzi Watatu walifariki dunia kutokana na vitendo vya utoaji Mimba kwa njia ya Kienyeji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo MAURICE SAPANJO amesema tatizo la mamba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo limeendelea kutokana na wazazi kushindwa kutoa ushirikiano kwa serikali dhidi ya watu wasababishaji wa ujauzito kwa wananfunzi.

NZOVWE. JIJINI MBEYA.

Sakata la aliyekuwa Diwani wa Chadema , Kata ya Nzovwe jijini Mbeya , Bwana HEZRON MWAKALOBO, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa kabla ya kuandika barua ya kujiuzuru, tayari, tayari alikabidhi kadi yake kwa katibu mkuu wa CCM mkoa , Bi VERENA SHUMBUSHO.

Mwakalobo alimkabidhi Katibu huyo kadi yake ya Chadema, yenye namba D.2009005150 Septemba 2 mwaka 2006.

Meya wa jiji la Mbeya, Bwana ATHANAS KAPUNGA WAKATI AKIZINGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI Mbeya amesema kuwa MWAKALOBO bado ni diwani halali wa kata hiyo na kuwa hajajiunga na Chama Cha Mapinduzi.

KAPUNGA amesema Julai 11, Mwaka huu , MWAKALOBO aliandika barua ya kujiuzuru nafasi hiyo aliyokuwa anaishikilia kwa tiketi ya CHADEMA, na kumkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya.

Ameongeza kuwa taarifa za kujiuzuru kwa diwani MWAKALOBO, zimekwishafikishwa kwa katibu mkuu wa TAMISEMI na kwa Mkurungezi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).

Kwa ushrikiano na mtandao wa -----UKURASA MPYA HUU Link (click here)http://ukurasampyahuu.blogspot.com/

Friday, June 24, 2011

DARAJA LA MUNGU RUNGWE

Wilaya Rungwe inavivutio vingi vya utalii, moja ya kivuti ambacho ni maajabu makubwa kwa dunia nzima ni Daraja la Mungu ambambalo unalitazama kwenye picha hiyo kama Umoja wa watangazaji mkoa wa Mbeya tunawakaribisha wadau mbalimbali kuja mkoa wa Mbeya na kutembelea vivutio hivyo muhimu na vyenye historia za ajabu hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Thursday, June 23, 2011

AKAMATWA NA KIGANJA CHA MTOTO MCHANGA NYUMBANI WAKE


JEMSI MAMBICHI mkazi wa kijiji cha Asamba wilayani Mbozi amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya akiwa na kiganja cha mtoto mchanga.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa nyumbani kwake ambapo kiungo hicho kilikuwa kimechimbiwa chini pembezoni mwa mlago wa chumbani kwake.

Kiungo hicho kimehifadhiwa hospitali ya Vwawa Mbozi kwaajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

Aidha kamanda NYOMBI amesema ELISHA AHONGA mwanafunzi wa shule ya msingi Sumbalwela amefariki dunia baada ya kupigwa na jiwe kichwani na NESTO MKONDYA mwanafunzi mwenzake wakati wakicheza mpira wa miguu shuleni hapo, mtoto huyo amekamatwa kwaajili ya uchunguzi zaidi.

WAFANYABIASHARA WASAMAKI MBEYA WATUMIA DAWA AINA YA ACCARICIDES KUHIFADHIA SAMAKI

Afisa afya mkoa wa Mbeya PETER MEREKI amesema kuwa wafanyabiashara wa samaki wa bichi watakaye bainika wanatumia dawa aina ya Accaricides ambayo inatumika kwa kilimo kuhifadhia samaki hao atachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuondoa hatari ya kiafya inayoweza kuwapata watumiaji wa samaki hao.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano na bomba fm na kusema kuwa mikoa ambayo inaongoza kwa wafanyabiashara kutumia dawa hiyo ni  Rukwa, Katavi na Mbeya


Wakati huohuo amewataka wananchi kutoa taarifa za haraka kwa vyombo vya sheria endapo watabaini kuwepo kwa wafanyabiashara wanaotumia dawa aina ya ACCARICIDES kwenye maeneo yao ili kuweza kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Wafanyabiashara hao wamekuwa wakitumia dawa hizo kwa madai kuwa inasaidia kuwakinga samaki wabichi wasiharibike mapema hata hivyo dawa hiyo ni sumu kwa afya ya binadamu.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HII LEO.

Leo ni siku ya wajane na Wagane Duniani ambapo wajane hupata fulsa  ya kutafakari majukumu muhimu walio achiwa na waumezao.

Akiongelea maadhimisho hayo wakili kutoka kituo cha msaada wa sheria (NOLA) Bwana SIMON NG’WIGULI amesema kisheria Mjane ni mrithi na mmiliki wa kwanza wa mali za Marehemu

Ameongeza kuwa mkoa wa Mbeya ni mmoja kati ya mikoa ambayo wajane wameathirika sana

Wakati huohuo ameimba serikali kuiadhimisha siku ya wajane kama inavyofanya kwenye maadhimisho mengine ili kutoa fulsa kwa wajane kujua haki zao za msingi.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HII LEO.